Ijumaa 3 Aprili 2026 - 15:00
Mhimili wa Muqawama bado haujafichua karata zake za kikanda

Hawza/ Katibu Mkuu wa Harakati ya Nujabaa, huku akirejea kushindwa kwa Marekani na utawala wa Kizayuni kufikia malengo yao katika vita vya Ramadhani, alisisitiza kwamba; mhimili huu bado haujafichua kadi zake za kikanda na una uwezo wa kuupa changamoto utawala wa adui katika eneo.

Kwa mujibu wa kitengo cha kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Akram al-Kaabi, Katibu Mkuu wa Harakati ya Nujabaa, aliandika katika mtandao wa kijamii wa X: “Huku mkiwamwagia mabomu mazito wanawake na watoto Waislamu, ghala la silaha la muqawama, kwa kutumia silaha rahisi, limeupa changamoto utawala wenu katika Mlango wa Hormuz na kuondoa eneo lenu la usalama.”

Licha ya kwamba Iran imekuwa chini ya mzingiro kwa miongo kadhaa, hamkuweza kulingana na ratiba mliojiwekea kwenye operesheni zenu za kijeshi, kupelekea Jamhuri ya Kiislamu kupiga magoti na wala hamkuweza kufanikisha hata moja ya malengo mliyoyatangaza mwanzoni mwa vita vyenu vya kishetani.

Je! Ikiwa mhimili wa muqawama ungetumia karata zake nyingine za kikanda, mngefanya nini?

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha